Hamas yatoa indhari kwa utawala haramu wa Kizayuni
(last modified Sun, 21 Oct 2018 23:18:51 GMT )
Oct 21, 2018 23:18 UTC
  • Hamas yatoa indhari kwa utawala haramu wa Kizayuni

Mshauri wa masuala ya habari wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameutahadharisha utawala wa Kizayuni dhidi ya kutenda jinai ya aina yoyote dhidi ya wananchi wa Palestina.

Taher al Nono amesema kuwa iwapo utawala wa Kizayuni utatenda jinai na uovu wowote dhidi ya wananchi wa Palestina; utawala huo utakabiliwa na radiamali ya wanamuqawama na kutoka kwa brigedi za shahidi Izzudin Qassam. 

Taher al Nono amesisitiza pia kuhusu maandamano ya haki ya kurejea yanayofanywa na raia wa Palestina huko Ukanda wa Ghaza na kubainisha kuwa: Maandamano hayo yalianza kama harakati ya wananchi tu kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Ghaza na yataendelea hadi malengo ya Wapalestina yatakapofikiwa. 

Vijana wa Kipalestina wakikabiliana na wanajeshi wa Israel katika maandamano ya haki ya kurejea

Maandamano ya haki za kurejea yalianza huko Ghaza tangu Machi 30 mwaka huu lengo likiwa ni kuhitimisha ukaliaji mabavu wa utawala wa Kizayuni na kuvunja mzingiro wa eneo hilo. Wapalestina zaidi ya 200 wameuliwa shahidi katika maandamano hayo na wengine zaidi ya elfu 22 wamejeruhiwa.    

Tags