Russia yakaribisha usitishaji vita Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4945-russia_yakaribisha_usitishaji_vita_yemen
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imekaribisha kutekelezwa usitishaji vita huko Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2016 23:50 UTC
  • Russia yakaribisha  usitishaji vita Yemen

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imekaribisha kutekelezwa usitishaji vita huko Yemen.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa Moscow iko tayari kusaidia mchakato wa kurejesha amani nchini humo.

Vilevile imetangaza kuwa katika mazingira ya sasa kufanyika jitihada za kuzuia kuvunjika usitishaji vita na kustafidi na mazungumzo ili kurejesha amani ya kudumu nchini Yemen ni suala lenye umuhimu mkubwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema inataraji kuwa juhudi za kurejesha amani huko Yemen zitazaa matunda.

Usitishaji vita upya huko Yemen umeanza kutekelezwa katika hali ya kulegalega kuanzia juzi Jumatatu ili kuandaa utangulizi wa mazungumzo ya amani.

Mazungumzo ya kusaka aman Yemen yamepangwa kufanyika huko Kuwait tarehe 18 mwezi huu.