Nov 29, 2018 03:09 UTC
  • Wanawake Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel wanadhalilishwa kijinsia na kuteswa

Wanawake Wapalestina ambao wameingizwa hivi karibuni katika jela ya utawala haramu wa Kizayuni ya Hasharon, katika eneo la Al-Damun, wamesema kwamba wanakabiliwa na mateso makubwa na kutusiwa huku haki yao ya kupatiwa huduma za kiafya ikipuuzwa na utawala huo.

Riyadh Al Ashqar, Msemaji wa Kituo Kinachojishughulisha na masuala ya Mateka wa Palestina amesema kuwa, tangu miaka 12 iliyopita hadi sasa mahakama za utawala wa Kizayuni zimetoa hukumu kali dhidi ya wanawake, ambapo wanawake wanane Wapalestina wamehukumiwa kifungo jela cha zaidi ya miaka 10 . Nasrin Abdullah Abukamil, mwanamke anayetoka Ukanda wa Gaza anatajwa kuwa katika hali mbaya sana ndani ya jela hiyo ambapo amekuwa akipatwa na maradhi ya kizunguzungu kila mara, utetemekaji mwili usiosita na kudhoofika kwa mishipa ya moyo na hivyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji.

Nasrin Abdullah Abukamil, Mfungwa mwanamke mwenye matatizo mengi ambaye amenyimwa huduma ya afya na Mazayuni makatili

Kwa mujibu wa habari hiyo licha ya kuwa na hali hiyo, utawala huo katili umepuuza kumpatia matibabu kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, huku akiwa amehukumiwa kifungo cha miaka sita. Taarifa ya Kituo Kinachojishughulisha na masuala ya Mateka wa Palestina kimeutaka Umoja wa Mataifa na asasi zinazowatetea wanawake na haki za binaadamu kufuatilia hali ya wanawake wa Palestina wanaoshikiliwa katika jela hizo za utawala haramu wa Israel. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, askari wa utawala huo wamewatia mbaroni wanawake na watoto wengi wa Kipalestina na kuwapeleka katika jela zake za kuogofya.

Tags