Jeshi la Syria latungua ndege nyingine ya Israel, makombora manne
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49856-jeshi_la_syria_latungua_ndege_nyingine_ya_israel_makombora_manne
Kikosi cha anga cha jeshi la Syria kimetungua ndege moja ya utawala wa Kizayuni wa Israel iliyoingia katika anga yake, kusini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 30, 2018 01:01 UTC
  • Jeshi la Syria latungua ndege nyingine ya Israel, makombora manne

Kikosi cha anga cha jeshi la Syria kimetungua ndege moja ya utawala wa Kizayuni wa Israel iliyoingia katika anga yake, kusini mwa nchi hiyo.

Televisheni ya al Alam imemnukuu afisa mmoja wa jeshi la Syria akithibitisha habari hiyo na kusema kuwa, kikosi cha anga cha jeshi la nchi hiyo usiku wa kuamkia leo kimejibu uvamizi wa anga wa adui Mzayuni katika mji wa al Kis'wah wa mkoa wa Rif Dimashq karibu na Damascus na kutungua ndege moja ya Israel pamoja na makombora manne yaliyolengwa na utawala huo vamizi.

Mfumo wa kujilinda na mashambulizi ya anga wa Syria

 

Afisa mmoja wa jeshi la Syria ameliambia shirika la habari la Sputnik la Russia kwamba mfumo wa kujilinda na mashambulizi ya anga wa Syria una uwezo wa kukabiliana vilivyo na shambulio lolote la anga la adui kama ambavyo una uwezo pia wa kutungua makombora yote ya adui kabla ya kufika yaliyokokusudiwa.

Mara kwa mara utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukifanya mashambulizi ya kivamizi ndani ya ardhi ya Syria ili kuyalinda magenge ya kigaidi na ya ukufurishaji kama vile Daesh (ISIS) na Jabhat al Nusra.

Syria imekumbwa na mgogoro tangu mwaka 2011 baada ya magaidi kumiminika nchini humo kutokea kila upande kwa msaada wa Saudi Arabia, Marekani, Israel na waitifaki wao, lengo kuu likiwa ni kujaribu kulinda usalama wa utawala wa Kizayuni unaokikalia kwa mabavu Kibla cha Kwanza cha Waislamu.