Askari katili wa Israel wamuua shahidi kwa risasi mwanamke wa Kipalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50812-askari_katili_wa_israel_wamuua_shahidi_kwa_risasi_mwanamke_wa_kipalestina
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limemuua shahidi kwa kumpiga risasi mwanamke wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 12, 2019 04:10 UTC
  • Askari katili wa Israel wamuua shahidi kwa risasi mwanamke wa Kipalestina

Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limemuua shahidi kwa kumpiga risasi mwanamke wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.

Ashraf al-Qedra, Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza amesema kuwa, mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina Aml Moustafa Ahmed (43) aliuawa shahidi akishiriki maandamano ya 42 ya kila Ijumaa ya "Haki ya Kurejea" yaliyofanyika jana katika mpaka wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza kuwa Wapalestina wasiopungua 25 wakiwemo watoto wadogo wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika maandamano hayo yaliyopewa kaulimbiu ya "Muqawama Wetu, Utavunja Mzingiro."

Askari wa Kizayuni wakiwafyatulia risasi waandamanaji wa Kipalestina Gaza

Maandamano ya amani yaliyopewa jina la "Haki ya Kurejea" yalianza tarehe 30 Machi mwaka uliopita kwa mnasaba wa Siku ya Ardhi huko Ukanda wa Gaza na yangali yanaendelea hadi sasa, licha ya ukandamizaji unaofanywa na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Wapalestina zaidi ya 240 wameuawa shahidi kufikia sasa, huku wengine 20,000 wakijeruhiwa katika maandamano hayo ya "Haki ya Kurejea".