Mar 13, 2019 13:50 UTC
  • Wakazi wa Al Mahrah, Yemen wapambana vikali na vibaraka wa Saudia

Watu wa makabila ya mkoa wa Al Mahrah nchini Yemen, wamepambana vikali na msafara wa malori yaliyobeba zana za kijeshi za Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mapigano hayo yameingia hatua ya utumiaji silaha kati ya pande mbili. Watu wa makabila ya mkoa huo wamekuwa wakilalamikia uvamizi wa askari wa Saudia katika mkoa huo wa mashariki mwa Yemen.

Mapigano yametokea baada ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Saudi Arabia kuwashambulia wakazi wa eneo hilo. Kabla ya hapo watu wa makabila ya mkoa wa Al Mahrah walipinga vibaraka wa Saudia kuweka kambi katika eneo la Shahan, ingawa hata hivyo matakwa yao hayakuheshimiwa na wavamizi wa eneo hilo.

Baadhi ya zana za kijeshi za Saudia zikiwa zimeteketezwa kwa moto

Mwezi April mwaka jana yaliwafanya askari vamizi wa kigeni na vibaraka wa Saudia walilazimika kuondoka katika kambi za kijeshi za eneo la al-Houf la mkoa huo kufuatia upinzani na maandamano ya wakazi hao.

Licha ya Saudia kwa kuungwa mkono katika mashambulizi yake nchini Yemen na Marekani, Israel, Uingereza, Ufaransa na baadhi ya nchi, lakini imeshindwa kuidhibiti nchi hiyo masikini ya Kiarabu kutokana na muqawama wa kishujaa wa wananchi Waislamu wa nchi hiyo.

Tags