Sheikh Abdul-Amir Qabalan: Mkutano wa Bahrain ni khiana kwa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57830-sheikh_abdul_amir_qabalan_mkutano_wa_bahrain_ni_khiana_kwa_palestina
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon ameulaani mkutano wa Bahrain na juhudi za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusema hatua yoyote ya kutaka kuanzisha uhusiano na Israel ni khiana kwa historia ya Uislamu na ardhi za Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 12, 2019 08:38 UTC
  • Sheikh Abdul-Amir Qabalan: Mkutano wa Bahrain ni khiana kwa Palestina

Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon ameulaani mkutano wa Bahrain na juhudi za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusema hatua yoyote ya kutaka kuanzisha uhusiano na Israel ni khiana kwa historia ya Uislamu na ardhi za Palestina.

Sheikh Abdul-Amir Qabalan amesisitiza kuwa, hatua ya kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel ni kupuuza kikamilifu damu za mashahidi na majeruhi wa muuqawama huko Palestina.

Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon ameeleza bayana kwamba, kufanyika huko Bahrain mkutano wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel ni juhudi zilizogonga mwamba za kutaka kumtambulisha adui badala ya rafiki na kuwasamehe watenda jinai.

Wakati huo huo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, utawala wa Aal Khalifa huko Bahrain umegeuka na kuwa mahala pa kupenyea Marekkani na utawala haramu wa Israel na kuingia katika umma wa Kiislamu na Kiarabu.

Sultan Qaboos wa Oman akiwa na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel

Hayo yanajiri katika hali ambayo, harakati za kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu zimeongezeka zaidi baada ya Benjamin Netanyahu kufanya safari nchini Oman Oktoba mwaka jana, hatua ambayo ilipelekea Oman iandamwe kwa ukosoaji mkubwa.

Hii ni katika hali ambayo, nchi za Kiarabu, Kiislamu na za ulimwengu kwa ujumla zimekuwa zikkitakiwa kufanya juhudi za kuuhami mji mtakatifu wa Quds unaokabiliwa na njama mbalimbali za Wazayuni maghasibu.