Baraza la Usalama latahadharisha kuhusu mashambulizi ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i5806-baraza_la_usalama_latahadharisha_kuhusu_mashambulizi_ya_kigaidi
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuhusu hatari ya kushadidi mashambulizi ya makundi ya kigaidi katika Bara Arabu na Iraq.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 26, 2016 04:42 UTC
  • Baraza la Usalama latahadharisha kuhusu mashambulizi ya kigaidi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuhusu hatari ya kushadidi mashambulizi ya makundi ya kigaidi katika Bara Arabu na Iraq.

Taarifa ilyotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imeeleza wasiwasi wake kuhusu kushadidi mashambulizi ya makundi ya kigaidi ya al Qaieda na Daesh katika Bara Arabu na Iraq na kutoa tahadhari kuhusu hali ya usalama ya Yemen.

Taarifa hiyo imesema, iwapo mazungumzo ya Kuwait hayatachunguza kwa kina muundo wa usalama wa Yemen, magaidi watatumia suala hilo kuzidisha mashambulizi yao. Baraza la Usalama pia limeyataka makundi, vyama na wananchi wote wa Yemen kuungana kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama wa nchi yao.

Mazungumzo ya amani ya Yemen yalisimamishwa Jumapili iliyopita nchini Kuwait na wajumbe wa harakati ya Ansarullah wanasema hawatashiriki tena katika mazungumzo hayo ila baada ya Saudi Arabia na washirika wake kusitisha kabisa mashambulizi ya anga dhidi ya raia wasio na hatia nchini Yemen.