Uturuki yaendelea kujizatiti kijeshi kinyume cha sheria kaskazini mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59050-uturuki_yaendelea_kujizatiti_kijeshi_kinyume_cha_sheria_kaskazini_mwa_syria
Jeshi la Uturuki limeendelea kujizatiti kaskazini mwa Syria baada ya kuingia msafara mpya wa kijeshi wa nchi hiyo katika mkoa wa Idlib.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 09, 2020 23:38 UTC
  • Uturuki yaendelea kujizatiti kijeshi kinyume cha sheria kaskazini mwa Syria

Jeshi la Uturuki limeendelea kujizatiti kaskazini mwa Syria baada ya kuingia msafara mpya wa kijeshi wa nchi hiyo katika mkoa wa Idlib.

Msafara mpya wa kijeshi kutoka Uturuki umevuka kivuko cha Babul-Hawa na kuingia mkoni  Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria. Jumamosi iliyopita pia jeshi la Uturuki lilihamishia mamia ya magari yake ya kijeshi katika mkoa huo, baada ya jeshi la serikali ya Syria kudhibiti moja ya miji ya kistratijia karibu na kitovu cha mkoa huo wa Idlib. Jeshi hilo vamizi la Uturuki limejenga vituo 12 vya kijeshi vya katika mkoa huo kwa kisingizio cha kupambana na wapiganaji wanaobeba silaha wa Kikurdi.

Uvamizi wa Uturuki dhidi ya nchi ya Syria

Kujizatiti huko kijeshi kwa Uturuki ndani ya ardhi ya Syria kunajiri katika hali ambayo, hatua ya askari wa nchi hiyo jirani ya kuingia hivi karibuni katika maeneo ya Syria kinyume cha sheria iliwafanya askari wa Syria kushambulia kwa mizinga maeneo ya askari hao vamizi ambapo kutokana na mashambulizi hayo askari kadhaa wa Uturuki waliuawa na wengine kujeruhiwa.