Syria yawakamata magaidi wanaofungamana na Marekani
Jeshi la Syria limetangaza kutekeleza oparesheni ambayo imepelekea kukamatwa wanachama wa kundi la kigaidi ambalo linafungamana na Marekani mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan, Jeshi la Syria jana Jumanne liliwanasa magaidi hao waliokuwa wakitoka katika kituo cha wanajeshi vamizi wa Marekani katika eneo la Al Tanf mashariki mwa Syria. Magaidi hao walikamatwa karibu na mji wa Al Sakhna, katika mkoa wa Homs mashariki mwa Syria.
Katika oparesheni hiyo magaidi watatu wa kundi hilo waliangamizwa na wengine kadhaa kukamatwa.
Marekani, ambayo imeingiza wanajeshi wake kinyume cha sheria kaskazini mashariki mwa Syria, si tu kuwa inaunga mkono magaidi bali pia inaendelea kupora utajiri wa mafuta ya Syria na vyanzo vingi vya asili vya nchi hiyo ya Kiarabu.
Serikali ya Syria imesisitiza mara kadhaa kuwa wanajeshi wa Marekani na waitifaki wake wako nchini Syria kwa lengo la kuikalia kwa mabavu nchi hiyo.