Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zashambulia Ukanda wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62882-ndege_za_kivita_za_utawala_wa_kizayuni_zashambulia_ukanda_wa_ghaza
Ndege za kivita za utawala haramu wa Kizayuni leo asubuhi zimeshambulia ngome za harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 18, 2020 03:00 UTC
  • Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zashambulia Ukanda wa Ghaza

Ndege za kivita za utawala haramu wa Kizayuni leo asubuhi zimeshambulia ngome za harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza.

Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amesema kuwa mashambulizi hayo ni jibu kwa kutumwa katika vitongoji vya Wazayuni maputo ya moto kutokea Ukanda wa Ghaza. 

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni jana usiku pia zilishambulia eneo la al Brij huko katikati mwa Ghaza. 

Mashambulizi ya Israel huko Ghaza  

Vijana wa Kipalestina siku kadhaa za karibuni walirusha vishada vya moto katiak ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu  wakilalamikia kuendelea kuzingirwa Ukanda wa Ghaza na Wazayuni.  

Ndege za kivita, helikopta, na makombora ya utawala wa Kizayuni katika miezi ya karibuni ziliyashambulia kwa mara kadhaa maeneo mbalimbali huko Ghaza.