Palestina yasisitiza kuvunja uhusiano na nchi zitakazohamishia balozi zao Baitul Muqaddas
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63263-palestina_yasisitiza_kuvunja_uhusiano_na_nchi_zitakazohamishia_balozi_zao_baitul_muqaddas
Katibu Mkuu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema, Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina itavunja uhusiano na nchi zitakazo hamishia balozi zao katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 06, 2020 23:05 UTC
  • Palestina yasisitiza kuvunja uhusiano na nchi zitakazohamishia balozi zao Baitul Muqaddas

Katibu Mkuu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema, Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina itavunja uhusiano na nchi zitakazo hamishia balozi zao katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem).

Saeb Erikat amesisitiza kuwa, kuhamishia balozi katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu kunakinzana na sheria za kimataifa.

Msemaji rasmi wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Nabil Abu Rudainah naye pia amesisitiza kuwa, Palestina inapata maana yake mji wake mkuu unapokuwa ni Baitul Muqaddas; na Marekani na utawala wa Kizayuni hawawezi kuubadilisha ukweli huo wa historia.

Saeb Erikat

Katika mwendelezo wa hatua za kuipiga vita Palestina, Rais Donald Trump wa Marekani, siku ya Ijumaa iliyopita alitangaza kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Kosovo na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na vile vile ahadi iliyotolewa na Serbia ya kuuondoa ubalozi wake ulioko Tel Aviv na kuuhamishia Baitul Muqaddas.

Hayo yanajiri wakati azimio nambari 478 la Umoja wa Mataifa linaeleza kwamba, ni marufuku na ni kinyume cha sheria kuchukua hatua yoyote ya kuanzisha asasi za kidiplomasia katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu; na linapinga pia hatua yoyote ya kubadilisha hali ya kisheria iliyopo katika mji huo wa Palestina.../