Wabunge Waarabu wapinga uhusiano wa kawaida wa Imarati na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64040-wabunge_waarabu_wapinga_uhusiano_wa_kawaida_wa_imarati_na_israel
Muungano wa wabunge Waarabu katika bunge la utawala wa Kizayuni (Kneset) wamepinga makubaliano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 15, 2020 23:08 UTC
  • Wabunge Waarabu wapinga uhusiano wa kawaida wa Imarati na Israel

Muungano wa wabunge Waarabu katika bunge la utawala wa Kizayuni (Kneset) wamepinga makubaliano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).

Mtandao wa habari wa "Arab24" umenukuu taarifa ya jana Alkhamisi ya Umoja wa Wabunge Waarabu katika bunge la utawala wa Kizayuni unaojulikana kwa jina la "Orodha ya Pamoja" ikisema kuwa, mpango wa "Muamala wa Karne" na makubaliano ya kutangaza uhusiano wa kawaida baina ya Imarati na Israel ni vitu ambavyo havikubaliki kabisa.

Muungano huo umesema kwamba hatua ya serikali ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ya kutekeleza Muamala wa karne na kutangaza uhusiano wa kawaida na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Imarati, ni maafa makubwa.

Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Tarehe 15 Septemba mwaka huu, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain walitia saini makubaliano ya kutangaza uhusiano wa kawaida baina ya nchi zao na utawala ghasibu wa Israel. Sherehe hizo zilizofanyika katika Ikulu ya Marekani, White House, zilihudhuriwa pia na rais wa Marekani, Donald Trump na Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.

Hati ya makubaliano hayo baina ya Imarati na utawala wa Kizayuni ilipasishwa Jumatatu wiki hii na Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni na ilitarajiwa kupigiwa kura jana Alkhamisi katika bunge la Israel.