Jeshi la Israel laanzisha mashambulizi dhidi ya kambi za Hamas, Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i6409-jeshi_la_israel_laanzisha_mashambulizi_dhidi_ya_kambi_za_hamas_gaza
Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limeshambulia kwa makombora minara ya kijeshi inayomilikiwa na harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 04, 2016 22:14 UTC
  • Jeshi la Israel laanzisha mashambulizi dhidi ya kambi za Hamas, Gaza

Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limeshambulia kwa makombora minara ya kijeshi inayomilikiwa na harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Kituo cha Habari cha Palestina kimesema hujuma hiyo ilifanyika jana Jumatano katika wilaya ya Shujaiyya katika Ukanda wa Gaza.

Habari zinasema kuwa, Izzudin Qassam, tawi la kijeshi la Hamas limejibu uchokozi huo kwa kushambulia kwa maroketi buldoza ya utawala haramu wa Israel katika wilaya hiyo. Duru za kiusalama za Palestina zimethibitisha kutokea mashambulizi hayo yaliyosababisha uharibifu mkubwa katika eneo ambalo liko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Palestina.

Ukanda wa Gaza umekuwa chini ya mzingiro wa utawala ghasibu wa Israel tangu Juni mwaka 2007. Mzingiro huo umefanya maisha ya Wapalestina kuzidi kuwa magumu huku wakazi wake wakikabiliwa na umaskini wa kupindukia.

Israel imeanzisha hujuma za kikatili mara tatu katika Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2008 yakiwemo mashambulizi ya mwaka 2014 ambayo yalisababisha mauaji ya Wapalestina 2,200 na wengine zaidi ya 11 elfu wakijeruhiwa.