Velayati: Syria imeimarika zaidi kuliko awali
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Kimataifa amesema kuwa Syria ya leo imeimarika zaidi kuliko hapo awali na kwamba uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu na Syria umekurubiana zaidi.
Dakta Ali Akbar Velayati ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria na kuongeza kuwa, Iran inaunga mkono mapambano ya wananchi na taifa la Syria dhidi ya ugaidi na makundi ya kitakfiri. Amesema uhusiano wa kidugu wa pande mbili na udharura wa kulindwa amani ya kanda hii unalazimu kuwepo mawasiiliano ya mara kwa mara kwa ajili ya kutathmini hali mambo.
Dakta Velayati amesifu misimamo ya Rais Bashar Assad wa Syria na kusema tadbiri na ushujaa vinaweza kuiongoza nchi hiyo na kuifikisha katika bara ya amani
Mshaui wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Kimataifa amewasili Syria baada ya kutembelea Lebanon ambako alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah.