Majeshi ya Yemen: Tutaendelea kupambana na wavamizi hadi ushindi wa mwisho
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65701-majeshi_ya_yemen_tutaendelea_kupambana_na_wavamizi_hadi_ushindi_wa_mwisho
Msemaji wa Majeshi ya Yemen amesisitiza kuwa wapiganaji wa nchi hiyo wataendelea kupambana na wavamizi hadi ushindi wa mwisho utakapopatikana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 10, 2021 21:11 UTC
  • Majeshi ya Yemen: Tutaendelea kupambana na wavamizi hadi ushindi wa mwisho

Msemaji wa Majeshi ya Yemen amesisitiza kuwa wapiganaji wa nchi hiyo wataendelea kupambana na wavamizi hadi ushindi wa mwisho utakapopatikana.

Brigedia Jenerali Yahya Saree jana Jumapili alieleza kuwa Marekani na Israel imeliweka jina la Yemen katika orodha ya nchi zinazozitia wasiwasi tawala hizo na kuongeza kuwa jambo hilo linaonyesha namna Yemen inavyoelekea katika njia sahihi, iwe ni katika kukabiliana na maadui au katika kupinga na kulaani suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni. 

Msemaji wa Majeshi ya Yemen wiki iliyopita pia aliyataja mafanikio ya kipekee ya kikosi cha makombora cha Yemen kuwa miongoni mwa fakhari za taifa la Yemen na kueleza kuwa: Kushindwa mtawalia kwa nchi vamizi ya Saudia kunadhihirisha udhaifu uliopo katika safu za wanajeshi vamizi wa nchi hiyo. 

Mwanajeshi vamizi wa Saudia aliyekamatwa mateka na askari wa Yemen 

Saudi Arabia na waitifaki wake wameshindwa kutimiza malengo yao huko Yemen ya kuiingiza madarakani serikali kibaraka kutokana na muqawama wa wananchi wa Yemen.