Jan 27, 2021 04:25 UTC
  • Wanajeshi wa Israel wamuua shahidi Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamempiga risasi na kumuua shahid kijana Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Arab24, tukio hilo limejiri Jumanne kusini mwa mji wa Nablus karibu na kitongoji cha Wazayuni cha Ariel kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan. Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamedai kuwa wamemuua kijana huyo kwa sababu akiwa anajaribu kutekeleza oparesheni ya kujitolea kufa shahidi. Wamedai kuwa kijana huyo aliwashambulia wanajeshi kadhaa wa Kizayuni kabla ya kupigwa risasi.

Siku ya Jumanne pia, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walimuua shahidi kijana Mpalestina karibu na Tulkaram, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

Katika kufikia malengo yao haramu ya kujitanua, kila siku huwashambulia Wapalestina na kuwajeruhi au kuwaua kwa madai mbali mbali mbali. 

Vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina

Kwa mujibu wa taasisi ya kutetea haki ya B'Tselem, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliwapiga risasi na kuwaua Wapalestina 27 mwaka uliopita wa 2020. Miongoni mwa waliouawa walikuwa ni watoto saba.

Aidha katika mwaka 2020, utawala dhalimu wa Israel ulibomoa majengo  729 ya Wapalestina na kuwaacha Wapalestina 1,006 bila makao wakiwemo watoto 519.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuzikoloni na kuzkalia kwa mabavu ardhi za Palestina kutokana na uungaji mkono wa Marekani na pia kutokana na kimya cha jamii ya kimataifa. 

Tags