Meli ya mizigo ya Israel yashambuliwa katika Bahari ya Hindi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71970-meli_ya_mizigo_ya_israel_yashambuliwa_katika_bahari_ya_hindi
Moto umezuka katika meli ya mizogo ya Israel baada ya kushambuliwa kwa 'silaha isiyojulikana' ikiwa katika maji ya Bahari ya Hindi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2021 02:44 UTC
  • Meli ya mizigo ya Israel yashambuliwa katika Bahari ya Hindi

Moto umezuka katika meli ya mizogo ya Israel baada ya kushambuliwa kwa 'silaha isiyojulikana' ikiwa katika maji ya Bahari ya Hindi.

Meli hiyo ilikuwa njiani kuelekea katika bandari ya Imarati iliposhambuliwa. Licha ya meli hiyo kusemekana kuwa ni ya Israel lakini viongozi wa utawala huo haramu wamesema wafanyakazi waliokuwemo hawakuwa raia wa utawala huo.

Televisheni ya N12 ya utawala wa Isreal imedai kuwa hakuna uharibifu mkubwa uliofanyika kwenye meli hiyo kufuatia shambulizi hilo na kwamba hakuna raia yeyote aliyejeruhiwa.

Meli ya mizigo ya utawala haramu wa Israel ikiwa katika maji ya Bahari ya Hindi

 

Mwezi Februari uliopita pia meli nyingine ya utawala wa Israel ilishambuliwa ikiwa katika maji ya Bahari ya Oman. Mwezi Aprili meli nyingine ya utawala huo ilishambuliwa katika pwani ya Umoja wa Falme za Kiarabu Imarati.