Wapalestina waandamana wakitaka Mahmoud Abbas ajiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71984-wapalestina_waandamana_wakitaka_mahmoud_abbas_ajiuzulu
Mamia ya Wapalestina wameandamana mjini Ramallah wakitaka Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas ajiuzulu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2021 08:43 UTC
  • Wapalestina waandamana wakitaka Mahmoud Abbas ajiuzulu

Mamia ya Wapalestina wameandamana mjini Ramallah wakitaka Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas ajiuzulu.

Wapalestina wameendeleza maandamana ya kulaani mauaji ya mwanaharakati wa Kipalestina Nizar Banat ambaye alikamatwa karibu ziku 10 zilizopita na vyombo vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Familia ya Banat pia nayo imeshiriki katika maandamano hayo ya amani. Huku wakiwa wamebeba picha za mwanaharakati huyo, waandamanaji wamesikika wakipiga nara dhidi ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambapo wametaka Mahmoud Abbas ajiuzulu. Waandamanaji wamemlaumu kwa kuhusika na mauaji ya Banat ambaye alikuwa mkosoaji wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Katika maandamano ya Jumamosi, maafisa wa usalama waliwazuia waandamanaji kufika katika makao makuu ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Mahmoud Abbas

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Nizar Banat alipoteza maisha baada ya kuteswa akiwa mikononi mwa maafisa wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Nizar Banat ni miongoni mwa raia wengine wengi ambao wamepoteza maisha wakiwa mikononi mwa polisi ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Banat alikuwa mwanaharakati wa kisiasa ambaye alipinga vikali kuhuishwa uhusiano wa malaka hiyo na utawala haramu wa Isreal. Kabla ya hapo mwanaharakati huyo alikamatwa mara kadhaa na polisi ya Malaka ya Ndani ya Palestina na kufungwa jela kutokana na upinzani wake dhidi ya suala hilo.