Ubalozi wa Marekani Baghadad washambuliwa tena kwa maroketi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i72134-ubalozi_wa_marekani_baghadad_washambuliwa_tena_kwa_maroketi
Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, umeshambuliwa tena kwa maroketi mapema leo Alhamisi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2021 06:28 UTC
  • Ubalozi wa Marekani Baghadad washambuliwa tena kwa maroketi

Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, umeshambuliwa tena kwa maroketi mapema leo Alhamisi.

Duru za usalama Iraq zinasema ubalozi huo wa Marekani ulio katika mtaa wa  Al-Khadhra umelengwa kwa maroketi ya Katyusha na kwamba mfumo wa kukabiliana na makombora ubalozini hapo umezuia maroketi hayo kutua.

Jumanne pia kulijiri shambulia dhidi ya jengo la ubalozi wa Marekani mjini Baghdad ambalo inasemakana lilitekelezwa kwa kutumia ndege isiyo na rubani au drone.

Aidha jana pia msafara wa majeshi ya Marekani kusini mwa Iraq ulilengwa kwa bomu la kutegwa ardhini katika barabara ya Basra na Dhi-Qar.

Msafara Wa wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq

Mashambulizi dhidi ya ubalozi na misafara ya wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq yangali yanaendelea huku Washington ikifanya kila iwezalo kuakhirisha mazungumzo ya kistratejia kati yake na Iraq kwa ajili ya kuondoa wanajeshi wake huko Iraq. 

Wananchi na makundi mengi ya Iraq yanataka kuondoka wanajeshi magaidi wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo. Bunge la Iraq pia tayari limepasisha mpango wa kuondoka wanajeshi hao nchini humo.