Wakimbizi wa Palestina waongezeka kwa asilimia 70 mwaka huu wa 2021
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i72464-wakimbizi_wa_palestina_waongezeka_kwa_asilimia_70_mwaka_huu_wa_2021
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema katika ripoti yake kuwa, idadi ya Wapalestina wanaolazimishwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuondoka kwenye makazi yao imeongezeka kwa asilimia 70 mwaka huu wa 2021.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 17, 2021 08:11 UTC
  • Wakimbizi wa Palestina waongezeka kwa asilimia 70 mwaka huu wa 2021

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema katika ripoti yake kuwa, idadi ya Wapalestina wanaolazimishwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuondoka kwenye makazi yao imeongezeka kwa asilimia 70 mwaka huu wa 2021.

Shirika la habari la IRNA limetangaza habari hiyiio leo Jumamosi na kuongeza kuwa, siku ya Jumatano pekee, Wapalestina 84 walipoteza nyumba zao huko Ramallah. Takwimu za awali za misaada ya kibinadamu zinaonesha kuwa, wanajeshi makatili wa Israel wamepora kwa uchache nyumba 49 za Wapalestina kwenye eneo hilo.

Jana Ijumaa pia, wanajeshi makatili wa Israel walivamia na kuvunja nyumba ya Mpalestina katika bonde la kaskazini mwa Mto Jordan na kuteka ardhi ya eneo hilo. Ripoti zinasema kuwa, nyumba hiyo ilikuwa ya familia ya watu wanane Wapalestina; wakiwemo watoto wadogo 6.

Jinai za wanajeshi wa Israel ni kubwa sana dhidi ya watoto wa Palestina

 

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2021 hadi hivi sasa, viongozi wa Israel wameharibu maeneo mengi sana ya Wapalestina. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wanajeshi madhalimu wa Israel wameharibu nyumba na maeneo 474 ya Wapalestina na kuwafanya wakimbizi wamiliki wa maeneo hayo.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Wapalesitna 656 wakiwemo watoto wadogo 359 wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wamefanywa wakimbizi na wanajeshi makatili wa Israel. Idadi hiyo inaonesha ongezeko la asimilia 70 ya wakimbizi wa Palestina na ongezeko la asilimia 75 ya watoto wa Kipalestina waliodhulumiwa na kufanywa wakimbizi na wanajeshi watenda jinai wa Israel. 

Cha kusikitisha ni kuona kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu, kama Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), zinazidi kujikomba kwa Wazayuni na kufungua balozi zao katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.