UN: Tunasikitishwa na kuongezeka jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa kwake na ongezeko la jinai za Israel dhidi ya Wapalestina.
Shirika la habari la IRIB limeinukuu ofisi ya uratibu wa masuala ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikiulaumu vikali utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema leo katika ripoti yake maalumu kwamba, katika kipindi cha wiki moja tu iliyopita, wanajeshi wa Israel wamewajeruhi Wapalestina 78 wakiwemo watoto wadogo 32 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia mbaroni 106 wengine.
Katika kipindi hicho pia, wanajeshi wa utawala vamizi wa Israel wamewateka nyara wavuvi 12 wa Kipalestina na kuwalazimisha waogelee hadi kwenye boti za wanajeshi hao katili.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, viongozi wa Israel wamepora nyumba 16 za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa madai ya eti hawakuwa na vibali vya kujenga.
Kuvunja nyumba na kupora ardhi za Wapalestina ni jambo la kawaida kwa utawala katili wa Kizayuni na lengo la viongozi wa Israel ni kuvuruga muundo wa kijamii na kijiografia wa maeneo ya Wapalestina.