Waislamu Uingereza waendesha kampeni maalumu za kuutambulisha Uislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7540-waislamu_uingereza_waendesha_kampeni_maalumu_za_kuutambulisha_uislamu
Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza imeitisha kikao maalumu cha kujibu maswali ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuhusiana na Uislamu na utamaduni wa Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 22, 2016 04:22 UTC
  • Waislamu Uingereza waendesha kampeni maalumu za kuutambulisha Uislamu

Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza imeitisha kikao maalumu cha kujibu maswali ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuhusiana na Uislamu na utamaduni wa Kiislamu.

Mtandao wa habari wa Ilford-recorder umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, katika kikao hicho cha kuutambulisha Uislamu kilichofanyika katika mji wa Ilford nchini Uingereza, kundi moja la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ohio cha Marekani nalo limealikwa na kuuliza maswali yaliyojibiwa katika kikao hicho kuhusiana na Uislamu.

Bashir Chaudhry, mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza amesema kwenye kikao hicho kwamba, jambo hilo limefanyika kwa lengo la kutoa mafunzo kuhusiana na tamaduni tofauti.

Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza amebainisha kuwa, baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Ulaya hususan huko Paris Ufaransa na Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji, Waislamu wamezidi kuandamwa na vitendo vya chuki za maadui wa Uislamu, kuliko wakati mwingine wowote ule.