Jan 22, 2022 08:47 UTC
  • Barham Salih: Shambulio la Diyala linaonyesha kushindwa magaidi nchini Iraq

Rais wa Iraq almesisitiza kuwa shambulio la kigaidi katika mkoa wa Diyala ni kitendo cha chuki kinacholenga usalama wa Iraq.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Rais wa Iraq Barham Salih amelaani shambulizi la kigaidi dhidi ya jeshi la nchi hiyo katika mkoa wa Diyala, akisema kuwa harakati za kufufua ugaidi katika eneo hilo hazipaswi kupuuzwa.

Salih ameongeza kuwa: "Wajibu wa maafisa wa nchi ni kuimarisha kambi ya ndani na kupiga hatua kwa mujibu wa katiba ili kuunda serikali yenye uwezo wa kulinda usalama wa taifa wa Iraq."

Wanajeshi 11 wa jeshi la Iraq waliuawa katika shambulio lililofanywa na kundi kigaidi la ISIS katika mkoa wa Diyala.

Licha ya serikali ya Iraq kutangaza mnamo mwezi Disemba 2017 kukombolewa kwa maeneo yote yaliyokuwa yamekaliwa kwa mabavu na magaidi wa ISIS, lakini mabaki ya kundi hilo bado yamejificha katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa, haswa katika mikoa ya Diyala, Al-Anbar, Salah al-Din na Ninawi. Magaidi hao hufanya operesheni za kigaidi za kushtukiza dhidi ya wanajeshi na raia wa Iraq.

Tags