Maandamano na kamatakamata zashtadi Bahrain katika maadhimisho ya vuguvugu la Mapinduzi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80286-maandamano_na_kamatakamata_zashtadi_bahrain_katika_maadhimisho_ya_vuguvugu_la_mapinduzi
Vyombo vya habari nchini Bahrain vimeripoti kuwa, sambamba na kuwadia mwaka wa 11 wa vuguvugu la mapinduzi ya Februari 14 ya wananchi wa Bahrain, yamefanyika maandamano katika maeneo mbalimbali, huku askari usalama wa utawala wa Aal Khalifa wakishadidisha kampeni ya kuwatia nguvuni wanaharakati wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 13, 2022 00:45 UTC
  • Maandamano na kamatakamata zashtadi Bahrain katika maadhimisho ya vuguvugu la Mapinduzi

Vyombo vya habari nchini Bahrain vimeripoti kuwa, sambamba na kuwadia mwaka wa 11 wa vuguvugu la mapinduzi ya Februari 14 ya wananchi wa Bahrain, yamefanyika maandamano katika maeneo mbalimbali, huku askari usalama wa utawala wa Aal Khalifa wakishadidisha kampeni ya kuwatia nguvuni wanaharakati wa nchi hiyo.

Maeneo kadhaa ya Bahrain yameshuhudia maandamano ya amani ya wananchi walioendeleza kilio chao cha kutaka uhuru na demokrasia katika nchi hiyo ya Kifalme.

Tovuti ya habari ya Mir-atul-Bahrain imeripoti kuwa, licha ya kusambazwa askari usalama katika mitaa na maeneo mbalimbali ya Bahrain kwa lengo la kuzuia maandamano na harakati za umma, maandamano yamefanyika katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Barbar, Abu Sabii n.k.

Hayo yanajiri huku wizara ya mambo ya ndani ya Bahrain ikishadidisha kampeni ya kuwakamata wapinzani na kuwaweka kizuizini sambamba na kukaribia siku ya maadhimisho ya vuguvugu la mapinduzi ya Februari 11, 2011.

Askari wa utawala wa Aal Khalifa wakikandamiza waandamanaji

Siku ya Alkhamisi, askari polisi waliwakamata vijana wawili Ali Jaafar Hussein na Ali Muhsin al Arab wa eneo la Bani Jamarah.

Mwaka wa 11 wa vuguvugu la mapinduzi ya Bahrain unaadhimishwa katika hali ambayo, kinyume na matakwa ya wananchi, uhusiano wa utawala wa kifalme wa Aal Khalifa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umestawi zaidi.

Wiki iliyopita, waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni Benny Gantz alielekea Manama ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Aal Khalifa na mrithi wa ufalme wake Salman bin Hamad.../