Qatar: Hatutoi gesi ya wateja wa Asia kwenda Ulaya
(last modified Wed, 19 Oct 2022 08:10:32 GMT )
Oct 19, 2022 08:10 UTC
  • Qatar: Hatutoi gesi ya wateja wa Asia kwenda Ulaya

Waziri wa Masuala ya Nishati wa Qatar ametangaza kuwa haitazamiwi katika msimu ujao wa baridi kali shehena ya gesi iliyopangwa kwenda Asia kuelekea Ulaya.

Suala la kuzidhaminia nchi za Ulaya nishati ya gesi limekuwa changamoto kuu katika miezi ya karibuni. Nchi za Ulaya ambazo zimeiwekea Russia vikwazo mbalimbali ili kuiweka chini ya mashinikizo nchi hiyo katika vita dhidi ya Ukraine sasa zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati ya mafuta na gesi. 

Vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia 

Saad bin Sherida al Kaabi Mkurugenzi wa Kampuni ya Nishati ya Qatar amesema kuwa nchi yake inaheshimu na kufungamana na ahadi na makubaliano iliyofikia kati yake na wateja na hakuna mpango wowote wa kutuma shehena ya gesi ya Asia kwa ajili ya nchi za Ulaya. 

Amesema, Kampuni ya Nishati ta Gesi ya Qatar inafanya juhudi ili kuwa kampuni kubwa zaidi ya gesi asilia duniani. Itafahamika kuwa, Qatar ni muuzaji mkubwa wa gesi asilia duniani na huku ikiwa imesaini makubaliano ya muda mrefu na Korea ya Kusini, Japan, India na China. 

Nchi za Ulaya zimeiwekea Russia vikwazo katika sekta ya nishati kwa kisingizo cha mashambulizi yaliyoanzishwa na nchi hiyo dhidi ya Ukraine na wakati huo huo vikwazo hivyo vimeibua changamoto kwa nchi hizo.