Jeshi la Israel laendelea kumwaga damu za Wapalestina Nablus
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89800-jeshi_la_israel_laendelea_kumwaga_damu_za_wapalestina_nablus
Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameendeleza umwagaji damu dhidi ya Wapalestina madhulumu katika mji wa Nablus ulioko katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu, na kuua shahidi wawili miongoni mwao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 29, 2022 00:24 UTC
  • Jeshi la Israel laendelea kumwaga damu za Wapalestina Nablus

Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameendeleza umwagaji damu dhidi ya Wapalestina madhulumu katika mji wa Nablus ulioko katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu, na kuua shahidi wawili miongoni mwao.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema Wapalestina hao waliouwa shahidi jana Ijumaa kwa kupigwa risasi na askari wa Kizayuni ni Imad Abu Rasheed (47) na Ramzi Sami Zabara (35).

Habari zaidi zinasema kuwa, Zabara na Abu Rasheed walikuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Ulinzi wa Umma ya Palestina, na walikuwa wakiishi katika kambi ya wakimbizi ya Askar, mashariki mwa viunga vya mji wa Nablus. 

Kabla ya hapo, jeshi hilo la Kizayuni lilifanya mashambulizi mengine na kuua shahidi Wapalestina sita mapema Jumanne lilipovamia mji huo wa kale wa Nablus na vile vile mji wa Ramallah ulioko kaskazini mwa Palestina.

Askari makatili wa Israel mjini Nablus

Utawala wa Kizayuni umeuweka mji wa Nablus chini ya mzingiro mkali kwa kisingizio cha kupanua operesheni zake dhidi ya wanamapambano wa Kipalestina katika eneo hilo na hasa uwepo wa wanachama wa kundi la mapambano la Arin al-Usud au 'Pango la Simba' katika mji huo.

Mzingiro na mashambulizi hayo hata hivyo yamejibiwa na makundi ya muqawama na wapigania uhuru wa Kipalestina hususan katika mji wa Nablus.