Kitivo cha utafiti cha Kizayuni: Israel ni jamii iliyosambaratika
Apr 19, 2023 02:24 UTC
Kitivo cha utafiti za Kizayuni cha masuala ya kimkakati na Kiusalama cha Baitul Muqaddas (Jerusalem) kinaitakidi kuwa, jamii ya Israel ni jamii iliyogawanyika na iliyoporomoka, na shaka na wasiwasi kuhusu misingi yake ya kimkakati unazidi kuongezeka siku baada ya siku.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, gazeti la Israel Hayom limenukuu ripoti ya Kitivo cha Israel cha masuala ya kimkakati na kiusalama ya Israel cha Quds na kuandika kuwa: jaribio la kuzifanyia mabadiliko sheria za mahakama limeisababishia Israel hasara isiyoweza kufidiwa.
Ripoti ya kituo hicho imeendelea kueleza: "hali ya Israeli imefikia hatua ambayo kila mtu kutoka nje anatuona kama jamii iliyosambaratika ambayo inapoteza polepole uwezo wake wa kufanya kazi".
Kwa mujibu wa ripoti ya kitivo cha masuala ya kistratejia na kiusalama cha Quds, nchi marafiki zilizotia saini makubaliano ya Abraham na Israel nazo pia zina shaka juu ya kuendelea kubakia kistratijia Israel katika eneo na zinafuatilia migogoro ya ndani ya utawala huo kwa mshangao, migogoro ambayo imepelekea wengine kuielezea kama hatari ya kuporomoka uwezo wa kijeshi wa Israel.
Inafaa kuashiria kuwa japokuwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu alisitisha mpango wa mabadiliko ya mahakama tangu mwezi uliopita wa Machi lakini maandamano ya upinzani dhidi yake na mipango yake yangali yanaendelea na Jumamosi iliyopita yaliingia katika wiki ya 15.../
Tags