Apr 25, 2023 01:25 UTC
  • HAMAS: Damu za mashahidi hazitaachwa kumwagika vivi hivi

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, kamwe haitoruhusu damu za mashahidi zimwagike vivi hivi. Taarifa ya harakati hiyo imetolewa baada ya wanajeshi makatili wa Israel kumuua kigaidi kijana mwingine wa Kipalestina huko Ariha.

Mapema jana asubuhi, wanajeshi magaidi wa Israel waliivamia kambi ya wakimbizi wa Palestina huko Ariha, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kumuua shahidi kijana wa Palesitna aliyejulikana kwa jina la Sulaiman Ayesh. Wanajeshi hao wa utawala wa Kizayuni wamemuua kijana huyo wa Kipalestina kwa kumpiga risasi na baadaye kuuiba mwili wake.

Tovuti ya al 'Ahd imenukuu taarifa ya harakati ya HAMAS ikisema kuwa, harakati hiyo itaendelea kushikamana vilivyo na ahadi zake za kupigania haki za Palesitna na mashahidi wa taifa hilo madhlumu ikiwa ni pamoja na damu ya shahid Sulaiman Ayesh iliyomwagwa jana Jumatatu na wanajeshi makatili wa Israel.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya HAMAS imesema kuwa, kambi za wakimbizi wa Palesina zinazoshuhudia jinai kubwa za mtawalia za Wazayuni, ndizo zitakazogeuka kuwa vituo vikuu vya mapambano ya ukombozi kama ambavyo ndivyo ilivyotokea hadi hivi sasa katika mapambano yote yaliyo dhidi ya Wazayuni. 

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS pia imesema, wananchi na vijana wanamapambano wa Palesina wataendeleza mapambano yao hadi watakapokomesha uvamizi wa kihayawani Wazayuni na kukombolewa kikamilifu Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Aprili hadi hivi sasa, makundi ya wanamapambano wa Palestina yameshafanya opereshenei zaidi ya 368 dhidi ya Wazayuni makatili.

Tags