-
Microsoft yalaaniwa kwa kumfuta kazi mhandisi aliyepinga mauaji ya kimbari Gaza
Apr 10, 2025 04:16Shirika moja la kimataifa limelaani hatua ya kampuni ya Microsoft ya Marekani kumfuta kazi mhandisi wa programu mwenye asili ya Morocco, Ibtihal Aboussad, ambaye aliandamana hadharani kupinga uungwaji mkono wa kampuni hiyo kwa utawala katili wa Israel wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Microsoft.
-
Wapalestina wengine 40 wauawa shahidi Gaza na mabomu ya Wazayuni
Apr 09, 2025 23:24Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kumwaga damu za Wapalestina; ambapo umewauwa Wapalestina karibu 40 wakiwemo watoto katika mashambulizi ya anga ya karibuni katika maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
-
Yemen yaangusha tena droni ya kisasa ya Marekani yenye thamani ya dola milioni 33
Apr 09, 2025 09:02Vikosi vya Yemen vimeangusha tena ndege ya kivita isiyo na rubani au droni ya kisasa aina ya MQ-9 ya Jeshi la Marekani iliyokuwa ikifanya "mashambulizi ya kijeshi" katika anga ya nchi hiyo.
-
Katibu Mkuu wa UN: Ghaza ni uwanja wa mauaji, kuwahamisha Wapalestina hakukubaliki
Apr 09, 2025 03:07Katika tamko kali zaidi ambalo amewahi kutoa hadi sasa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa indhari kuhusu hali ya janga la kibinadamu inayozidi kuwa mbaya katika Ukanda wa Ghaza.
-
Hamas yafananisha vitendo vya Israel Gaza na mauaji ya kimbari ya Rwanda
Apr 08, 2025 23:35Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imefananisha vitendo vya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya kimbari ya Rwanda, huku ikisifu hatua ya Umoja wa Afrika ya kumfukuza balozi wa utawala wa Israel kutoka mkutano maalumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
-
Israel yampiga marufuku mkurugenzi wa Msikiti wa Ibrahimi kwa siku 15
Apr 08, 2025 23:02Utawala haramu wa Israel umempiga marufuku mkurugenzi wa Msikiti wa Ibrahimi ulioko katika mji wa al-Khalil, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kuingia katika eneo hilo takatifu la Kiislamu kwa zaidi ya wiki mbili, huku utawala huo ukiendeleza mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.
-
Ndege za kivita za Marekani zashambulia Yemen karibu mara 30 katika muda wa chini ya siku moja
Apr 08, 2025 06:47Marekani imefanya karibu mashambulizi 30 ya anga katika majimbo kadhaa kote nchini Yemen katika muda wa chini ya siku moja, na kushadidisha uchokozi wake dhidi ya taifa hilo, katika kile ambacho wataalamu wamekitaja kuwa ni harakati za kujishinda yenyewe za kusitisha bila mafanikio operesheni za Sana'a zinazotekelezwa dhidi ya Israel na waungaji mkono wake kwa ajilii ya kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Mashirika sita ya UN: Vita vya Ghaza ni ishara ya kutojaliwa hata chembe maisha ya binadamu
Apr 08, 2025 06:21Wakuu wa mashirika sita ya Umoja wa Mataifa wametoa indhari kali kuhusu hali ya Ukanda wa Ghaza na kutaka usitishaji vita utekelezwe tena na kwa haraka sana, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya katika eneo hilo linaloendelea kuandamwa na mashambulio ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Msemaji wa Taliban: Askari wa Marekani hawawezi kuruhusiwa kuwepo ndani ya ardhi ya Afghanistan
Apr 08, 2025 06:11Msemaji wa serikali ya muda ya Afghanistan amesisitiza kuwa haiwezekani askari wa Marekani waruhusiwe kwenda na kuwepo ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Waisraeli waandamana kupinga kuanza tena vita vya Gaza
Apr 08, 2025 03:11Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya Tel Aviv kushiriki katika maandamano mapya ya kupinga serikali ya utawala haramu wa Israel, wakati ambapo Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu alipokutana na Rais wa Marekani, Donald Trump mjini Washington.