-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Syria na Oman wawasiliana kujadili matukio ya Asia Magharibi
Apr 28, 2023 03:28Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Syria na Oman wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya kikanda.
-
Mkuu wa Kamisheni ya EU atakiwa aombe radhi kwa 'ukanushaji wa kibaguzi' kuhusu Nakba
Apr 27, 2023 08:15Palestina imelaani matamshi ya chuki aliyotoa Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 75 wa kuundwa utawala haramu na bandia wa Israel na kumtaka atoe kauli ya kuomba radhi.
-
Iran ina azma ya kurejesha uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na Saudi Arabia
Apr 27, 2023 07:22Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda, Migodi na Kilimo cha Iran (ICCIMA) ametoa wito wa kurejeshwa kwa haraka uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na Saudi Arabia na kukuzwa ushirikiano kati ya wafanyabiashara na wenye viwanda vya sekta binafsi za nchi hizo mbili.
-
Hamas: Maonyo ya Sayyid Nasrullah ndiyo sababu kuu ya woga wa utawala wa Kizayuni
Apr 27, 2023 02:07Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, maonyo yanayotolewa na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah ndiyo sababu kuu inayozuia mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Indhari kuhusu njama ya Israel ya kugeuza eneo la Kiislamu la Bab Al-Rahma kuwa Sinagogi
Apr 26, 2023 23:33Kundi la kutetea haki za binadamu limeonya kuhusu njama ya utawala ghasibu wa Israel kugeuza Jumba la Sala la Bab Al-Rahma katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa sinagogi.
-
Maandamano ya maelfu ya Wazayuni yanaendelea katika ardhi za Palestina
Apr 26, 2023 02:48Maelfu ya Wazayuni wameendelea na maandamano yao ya kumpinga waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, katika miji ya Quds na Tel Aviv licha ya kuweko sherehe za miaka 75 ya kuasisiwa utawala haramu na pandikizi wa Israel.
-
Balozi Zawawi: Muda wa kukombolewa taifa la Palestina umewadia
Apr 25, 2023 22:33Balozi wa Palestina nchini Iran amesema kuwa, umewadia wakati sasa kwa taifa la Palestina kukombolewa na sote tuswali katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.
-
Mapatano ya Iran na Saudia yamefungua mlango wa msururu wa maridhiano katika eneo
Apr 25, 2023 09:00Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kistratejia cha mjini Sana'a amesema, mapatano yaliyofikiwa kati ya Saudi Arabia na Iran yatakuwa na taathira chanya kwa masuala muhimu ya eneo, kadhia ya Yemen ikiwa mojawapo ya masuala hayo.
-
Kuanza tena mashambulizi ya Wazayuni kwenye Msikiti wa Al-Aqsa baada ya Ramadhani
Apr 25, 2023 00:12Mivutano mipya inazuka katika Msikiti wa Al-Aqsa sambamba na kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
HAMAS: Damu za mashahidi hazitaachwa kumwagika vivi hivi
Apr 24, 2023 21:55Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, kamwe haitoruhusu damu za mashahidi zimwagike vivi hivi. Taarifa ya harakati hiyo imetolewa baada ya wanajeshi makatili wa Israel kumuua kigaidi kijana mwingine wa Kipalestina huko Ariha.