-
Palestina: Hatutakubali msikiti wa Al-Aqsa ugawanywe kimatumizi kwa wakati na eneo
Apr 06, 2023 03:55Mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema: Hatutakubali msikiti wa Al-Aqsa ugawanywe kimatumizi kwa sura ya muda maalumu wa utumiaji na sehemu maalumu ya kutumia jambo ambalo wavamizi na walowezi wa Kizayuni wanapigania kulilazimisha liwe.
-
Wairaqi zaidi ya milioni moja wametoweka na hawajulikani waliko
Apr 05, 2023 07:55Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kuwa, zaidi ya watu milioni moja wametoweka nchini Iraq na hawajulikani waliko; katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita, ikiwa ni pamoja na enzi za udikteta wa Saddam Hussein, za uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani, na za kuibuka kwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).
-
Kwa nini Israel inaogopa kuboreshwa uhusiano kati ya Iran, Syria na nchi za Kiarabu?
Apr 05, 2023 06:41Kuboreka uhusiano kati ya Syria na nchi za Kiarabu katika siku za hivi karibuni, hasa na Saudi Arabia, ambako kumefungua mlango wa kushiriki Rais wa Syria, Bashar Assad, katika mkutano ujao wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) huko Riyadh, kumeitia kiwewe na wasiwasi wa utawala ghasibu wa Israel.
-
UN yapasisha azimio la kuwatetea Wapalestina katika Baraza la Haki za Binadamu
Apr 04, 2023 09:57Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuwatetewa Wapalestina, ambalo limekaribishwa na Wapalestina.
-
Ugaidi; mbinu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kujinasua na migogoro ya ndani
Apr 04, 2023 06:33Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuuawa shahidi washauri wawili wa kijeshi wa Iran katika mashambulizi ya anga dhidi ya Syria na kueleza kwamba, hatua za kigaidi hazitabakia bila majibu.
-
Tel Aviv yatiwa wasiwasi na kuboreshwa uhusiano wa Syria na nchi za Kiarabu
Apr 04, 2023 04:18Taasisi za usalama na masuala ya siasa za utawala wa Kizayuni zimebainisha wasiwasi wo kuhusu kukaribia kuhuishwa uhusiano kati ya Syria na Misri na nchi nyinginen za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.
-
Wapalestina 2 wauawa shahidi, 16 wajeruhiwa huko Nablus
Apr 04, 2023 03:37Shirika la Huduma za Dharura la Mwezi Mwekundu la Palestina limetangaza kuwa Wapalestina 2 wameuawa na 16 kujeruhiwa katika mapigano jana Jumatatu na wanajeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni huko Baita kusini mwa mji wa Nablus.
-
Chama cha ushirika cha wafanyabiashara wa Iran na Saudia kuzinduliwa hivi karibuni
Apr 03, 2023 22:42Mjumbe wa bodi ya uongozi ya Chama cha Wafanyabiashara wa Iran amesema, sekta binafsi imeanza kuandaa mipango inayohitajika kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi na Saudi Arabia, na akabainisha kwamba chama cha ushirika cha Wafanyabiashara wa Iran na Saudi Arabia kitazinduliwa hivi karibuni.
-
Saudia yamwalika Rais Assad wa Syria katika kikao cha Riyadh cha viongozi wa Arab League
Apr 03, 2023 22:41Shirika la habari Reuters limeripoti kuwa, Saudi Arabia inapanga kumualika Rais Bashar al-Assad wa Syria kuhudhuria mkutano ujao wa wakuu wa nchi za Kiarabu.
-
Kulalamikia Chama cha Tahreek-e-Insaf uhusiano wa kibiashara wa Pakistan na utawala haramu wa Israel
Apr 03, 2023 22:40Chama cha Tahreek-e-Insaf cha Pakistan kimelalamikia kuweko uhusiano wa biashara ya bidhaa za chakula baina ya nchi hiyo na utawala haramu wa Israel na kimeitaka Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo kutoa maelezo kuhusiana na suala hilo.