Oct 05, 2023 13:10 UTC
  • Rais Putin: Uhusiano wa Russia na Iran ni 'mzuri mno'

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema uhusiano wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mzuri na wa kuridhisha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, Rais Putin amesema hayo katika mji wa kitalii wa Sochi, kaskazini magharibi mwa Russia na kuongeza kuwa, Moscow itafanya kila iwezalo kuimarisha uhusiano wake na Tehran.

"Tuna uhusiano mzuri sana na Iran na tutafanya juu chini kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa mataifa haya," ameeleza Rais Putin.

Rais wa Russia amebainisha kuwa, nchi hiyo ina hamu ya kuanzisha taasisi za kielimu nchini Iran, ambazo zitatoa mafunzo kwa kutumia Kirusi na kwa mujibu wa mitaala na mifumo ya nchi hiyo.

Marais wa Iran na Russia

Jumanne usiku, Rais Putin alizungumza na mwenzake wa Iran, Ebrahim Raisi kwa njia ya simu, ambapo walijadiliana juu ya mahusiano ya pande mbili ya Moscow na Tehran.

Sayyid Raisi alisema anaridhishwa na kiwango cha uhusiano na ushirikiano baina ya Iran na Russia, huku akitoa mwito wa kutekelezwa haraka miradi ya pamoja ya nchi mbili hizi, hasa katika nyuga za miundombinu na nishati.

Tags