Oct 18, 2023 06:33 UTC
  • Radiamali ya Rais Putin kuhusu matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani

Rais wa Russia amesema katika radiamali yake kuhusiana na matamshi ya hivi karibuni ya Rais Joe Biden wa Marekani kwamba Marekani lazima ijifunze jinsi ya kuheshimu wenzake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, Rais Vladimir Putin wa Russia alisema Jumanne akijibu maoni ya hivi karibuni ya Joe Biden aliyedema kuwa Vladimir Putin anapaswa kuondolewa madarakani, kwamba rais huyo anapaswa kujifunza jinsi ya kuheshimu wenzake na hawapaswi kumdhalilisha mtu yeyote kivyovyote vile.

Putin ameongeza kuwa kuwadhalilishaji wengine mara kwa mara huibua matatizo. Viongozi wa Marekani hutabasamu na kupeana mikono wakati wa hafla za sherehe, lakini kwa kweli, hawaheshimu watu wala mataifa, na hufanya hivyo tu kwa ajili ya kulinda masilahi yao.

Akiashiria kuwa masilahi ya Russia hayawezi kukandamizwa, Putin amesema kwamba Warussia wanapaswa kuheshimiwa.

Wakati huohuo, Dmitry Peskov, Msemaji wa Ikulu ya Russia, amesema akijibu madai ya Rais wa Marekani Joe Biden kwamba iwapo majeshi yote ya Ulaya yataungana, yatamshinda Rais Vladimir Putin, kuwa matamshi hayo si mapya na kuwa kufikia sasa viongozi wa Magharibi hawajafanikiwa na wala hawatafanikiwa katika katika uwanja huo.

Dmitry Peskov Msemaji wa Ikulu ya Russia

Dmitry Peskov amesema kuwa Biden na viongozi wa Ulaya wanatumia pesa zao bure, na kuongeza kuwa Wamagharibi wanadai kuwa wanataka kumshinda Putin na Russia, lakini hawajafanikiwa na hawatafanikiwa.

Awali, Biden alidai katika mahojiano na CBS kwamba Washington inaweza kuunganisha Ulaya yote, kuinyima Russia uhuru wa utendaji na kumshinda rais wa nchi hiyo.

Tags