Feb 23, 2024 11:22 UTC
  • Cuba yalaani sera za mauaji ya kimbari za utawala haramu wa Israel

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Cuba amelaani kuendelea uvamizi na mauaji ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kusema: Israel imepitisha "sera ya kuwaangamiza" wananchi wa Palestina.

Bruno Rodríguez Parrilla, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Cuba amesema hayo katika ujumbe wake aliochapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamiii wa X na kueleza kwamba, maelfu ya watu katika Ukanda wa Gaza wanahitajia msaada wa huduma ya afya.

Wakati huo huo Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel akizungumzia kura ya turufu ya Marekani dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Gaza amesema: Washington ni mshirika wa Tel Aviv katika maafa ya mauaji ya kimbari ya watu wa Palestina.

Katika upande mwingine, Uingereza ambayo nayo ni moja ya waungaji mkono wakuu wa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina sambamba na Ujerumani na Marekani, hivi sasa imetoa idhini mpya kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina hasa wa Gaza.

Zaidi ya Wapalestina 28,000 wameuawa Gaza tangu Israel ilipoanzisha mashambulio ya kinyama Oktoba 7, 2023

Idhini hiyo inafuatia hatua ya Mahakama Kuu ya London, kukataa ombi la kuiamrisha serikali ya Uingereza iache kuipatia silaha Israel.

Mwaka 2022, Uingereza iliipa Israel silaha zenye thamani ya dola milioni 53 vikiwemo vipuri vya ndege, zana za kivita, makombora pamoja na silaha nzito na nyepesi.

Madola hayo matatu ya Magharibi ndiyo yaliyoko mstari wa mbele katika kuusheheneza silaha hatari utawala wa Kizayuni ili uzidi kuua raia wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.

Tags