Mataifa masikini bado yanayumba baada ya UVIKO 19
https://parstoday.ir/sw/news/world-i109498-mataifa_masikini_bado_yanayumba_baada_ya_uviko_19
Ripoti ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa imesema kuwa, mataifa mengi hivi sasa yanarejea katika hali ya kawaida baada ya janga la UVIKO-19, ingawa mataifa masikini zaidi yanazidi kudidimia.
(last modified 2024-03-14T09:21:09+00:00 )
Mar 14, 2024 09:21 UTC
  • Mataifa masikini bado yanayumba baada ya UVIKO 19

Ripoti ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa imesema kuwa, mataifa mengi hivi sasa yanarejea katika hali ya kawaida baada ya janga la UVIKO-19, ingawa mataifa masikini zaidi yanazidi kudidimia.

Mkuu wa mpango huo Achim Steiner amesema kwamba, utafiti huu ni ishara ya wazi kwamba pengo hivi sasa linaongezeka baada ya miongo miwili kuliposhuhudiwa mataifa tajiri na masikini yakikaribiana kimaendeleo.

Faharasa ya Maendeleo ya Kibinadamu ya shirika hilo ya tangu 1990 imeonyesha kuwa, maendeleo kwenye nusu ya mataifa masikini zaidi yameendelea kuwa chini ya viwango vilivyokuwepo hata kabla ya UVIKO.

Mataifa hayo yenye viwango vya chini zaidi kuanzia mwaka 2022 yalikuwa ni Sierra Leone, Burkina Faso, Yemen, Burundi, Mali, Chad, Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini and Somalia.

 

Mwezi Mei mwaka jana Mkurugenzi Mkuu wa WHO Data Tedros Adhanom Gebreyesus pia juzi alitangaza kufikia kikomo hali ya dharura ya maambukizi ya corona. Dakta Tedros alisisitiza kuwa hii haimaanishi kumalizika tishio la virusi vya corona bali bado kuna hatari ya kubadilika upya virusi hivyo.

Takwimu zinaonyesha kuwa, sasa zaidi ya watu milioni saba na laki wameaga dunia kwa ugonjwa wa Uviko-19 duniani na kwamba kuna uwezekano takriban watu milioni 20 walikufa kwa ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya Duniani anayehusika na Dharura za Kiafya ameeleza kuwa kuna vigezo maalumu sana na vya kipekee kwa ajili ya kutokomeza virusi vya corona na kwamba ni vigumu kutokomeza kabisa virusi hivyo.