Kidole cha shahada cha Rudiger chatumiwa kuwashambulia Waislamu Ujerumani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i110046-kidole_cha_shahada_cha_rudiger_chatumiwa_kuwashambulia_waislamu_ujerumani
Kundi lenye siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani limezusha mzozo mkubwa nchini humo baada ya kumhusisha mchezaji wa soka Muislamu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Antonio Rudiger, na "makundi ya kigaidi" kwa sababu tu ameonekana kwenye picha ya Instagram akiwa amevaa kanzu nyeupe juu ya mswala, akiinua juu kidole chake cha shahada.
(last modified 2024-03-29T22:58:14+00:00 )
Mar 29, 2024 22:58 UTC
  • Kidole cha shahada cha Rudiger chatumiwa kuwashambulia Waislamu Ujerumani

Kundi lenye siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani limezusha mzozo mkubwa nchini humo baada ya kumhusisha mchezaji wa soka Muislamu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Antonio Rudiger, na "makundi ya kigaidi" kwa sababu tu ameonekana kwenye picha ya Instagram akiwa amevaa kanzu nyeupe juu ya mswala, akiinua juu kidole chake cha shahada.

Mzozo huo umetokea baada ya Julian Reichelt, aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Bild, kumtuhumu Antonio Rudiger kuwa ana uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh.  Mchezaji huyo pamoja na Shirikisho la Soka la Ujerumani wameachukua hatua ya kumfungulia kesi mwandishi huyo wa habari kwa tuhuma za kutoa matamshi ya chuki, kashfa na uchochezi.

Picha hiyo ya Antonio Rudiger iliambatana na maneno: "Ramadan Mubarak kwa Waislamu wote. Mungu atukubalie Saumu na maombi yetu," na ilichapisha mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Antonio Rudiger

Mwandishi huyo wa habari amedai kwamba, kitendo cha kutoa shahada cha Rüdiger "ni nembo ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) na eti wauaji wa Kiislamu duniani kote."

Reichelt anajulikana kwa misimamo yake ya kuiunga mkono Israel anapochapisha jumbe kila siku kwenye mtandao wa X ambazo zinaangazia simulizi rasmi za utawala unaoendelewa huo kuua watoto wa Palestina.

Abdul Samad Al-Yazidi, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani anasema: "Wale walioanzisha kashfa hii wanajua kwa hakika kwamba kuinua kidole cha shahada hakuna uhusiano wowote na kundi la kigaidi la ISIS, bali ni ishara ya imani ya Tauhidi na Mungu Mmoja, lakini wanajaribu kutengeneza migogoro ili kuchochea umma dhidi ya Waislamu."