Jun 03, 2024 08:08 UTC
  • Mexico yapata Rais wa kwanza mwanamke; ni Sheinbaum

Claudia Sheinbaum amechaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchiini Mexico katika ushindi wa kihistoria.

Mamlaka rasmi ya uchaguzi ya Mexico imesema kuwa, matokeo ya awali yameonyesha kuwa Sheinbaum meya wa zamani wa Mexico City mwenye umri wa miaka 61 ameshinda kati ya 58% na 60% ya kura katika uchaguzi wa jana Jumapili.

Matokeo hayo yanampa mwanamama huyo uongozi wa zaidi ya asilimia 30 ya pointi zaidi ya mpinzani wake mkuu, mfanyabiashara Xóchitl Gálvez.

Bi Sheinbaum atachukua nafasi ya Rais anayemaliza muda wake Andrés Manuel López Obrador, tarehe 1 Oktoba.

Wapiga kura pia walikuwa wakiwachagua wajumbe wote wa Bunge la Mexico na magavana katika majimbo manane, pamoja na mkuu wa serikali ya Mexico City. Ripotii zinaeleza kuwa, kampeni za uchaguzi huo zilikumbwa na mashambulizi makali.

Serikali inasema zaidi ya wagombea 20 wa eneo hilo wameuawa kote Mexico, ingawa tafiti za kibinafsi zinaweka jumla ya 37 waliuawa.

Watu wawili waliripotiwa kuuawa katika mashambulizi mawili kwenye vituo vya kupigia kura katika jimbo la Puebla siku ya Jumapili, maafisa wa serikali walisema.

Tags