Waziri Mkuu wa Denmark ashambuliwa na kupigwa Copenhagen
https://parstoday.ir/sw/news/world-i112688-waziri_mkuu_wa_denmark_ashambuliwa_na_kupigwa_copenhagen
Waziri Mkuu wa Denmark Bi Mette Frederiksen alishambuliwa jana Ijumaa alipokuwa kwenye bustani ya Copenhagen, mji mkuu wa nchi hiyo.
(last modified 2024-06-08T07:40:37+00:00 )
Jun 08, 2024 07:40 UTC
  • Waziri Mkuu wa Denmark ashambuliwa na kupigwa Copenhagen

Waziri Mkuu wa Denmark Bi Mette Frederiksen alishambuliwa jana Ijumaa alipokuwa kwenye bustani ya Copenhagen, mji mkuu wa nchi hiyo.

Shambulio hilo limethibitishwa ofisi yake.

Ofisi Waziri Mkuu huyo Bi Mette Frederiksen imeziambia duru za habari kwamba Waziri Mkuu huyo alipigwa na mtu mmoja Ijumaa jioni katika eneo la Kultorvet mjini Copenhagen na kuongeza kuwa ameshtushwa na tukio hilo, ingawa haikueleza zaidi.

Taarifa zaidi zinasema, vyombo vya usalama vilifanikiwa kumtia mbaroni mtu huyo.  Hata hivyo hadi sasa haijafahamika sababu hasa iliyompelekea mtu huyo amshambulie Waziri Mkuu huyo.

Viongozi mbalimbali wa Ulaya wamelaani vikali shambulio hilo. Mkuu wa Umoja wa Ulaya Charles Michel pamoja na Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola wamelaani shambulizi hilo dhidi ya Frederiksen.

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ambaye hivi karibuni alishambuliwa kwa kupigwa risasi

Tukio hili linatokea katikati ya ongezeko la mashambulizi dhidi ya wanasiasa wakiwa kazini ama kwenye kampeni nchini Ujerumani kabla ya uchaguzi wa wabunge wa Umoja wa Ulaya wiki hii.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico alipigwa risasi kadhaa  katika jaribio la kumuu na alijeruhiwa vibaya na kufanyiwa upasuaji.