Uchunguzi wa Pew: Wamarekani weusi, wahanga wa ubaguzi wa rangi
Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha kuwa, Wamarekani wengi weusi wanaamini kuwa ni wahanga wa ubaguzi wa rangi.
Uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na taasisi ya Pew unasema kuwa asilimia 65 ya raia weusi wa Marekani wanaamini kuwa maisha ya Mmarekani mweusi ni magumu zaidi mara dufu kuliko maisha ya raia mzungu, na asilimia 27 ya Wamarekani weupe wamesema wanakubaliana na mtazamo huo.
Katika uchunguzi huo wa maoni uliofanyika kote nchini Marekani katika kipindi cha kati ya tarehe 7 Juni hadi 5 Julai mwaka huu, zaidi ya thuluthi moja ya Wamarekani wenye asili ya Latini America wamethibitisha kuwa, maisha ya mtu mweusi nchini Marekani ni magumu zaidi kuliko maisha ya wazungu na watu weupe.
Polisi ya Marekani inalaumiwa kwa kuwalenga kwa risasi raia wenye asili ya Afrika kwa sababu za kibaguzi.