Takriban watoto milioni 500 wanaishi katika maeneo yenye migogoro duniani
(last modified Thu, 31 Oct 2024 07:03:21 GMT )
Oct 31, 2024 07:03 UTC
  • Takriban watoto milioni 500 wanaishi katika maeneo yenye migogoro duniani

Katika ripoti yake ya hivi karibuni inayoitwa Stop the War on Children, taasisi ya Save the Children imeripoti ongezeko la asilimia 14 ya vitendo vya ukiukaji wa haki za watoto wanaoishi katika maeneo yenye migogoro duniani kote kwa mwaka 2023.

Zaidi ya kesi 31,000 zimerekodiwa mwaka huu yaani takriban kesi 86 za unyanyasaji kila siku ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono, na mashambulizi dhidi ya shule.

''Zaidi ya watoto milioni 473 yaani zaidi ya theluthi moja ya idadi ya watu duniani wanaishi katika maeneo yenye migogoro hivi sasa. Mwaka 2023 pia, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto yaani kesi 31,729 kama zinavyoonesha takwimu za Umoja wa Mataifa.

Musa Chibwana, Mchambuzi wa Misaada ya Kibinadamu katika Shirika la Save the Children amesema kuwa, Ukiukwaji huo ni pamoja na idadi ya kutisha ya mauaji na ukeketaji.

Watoto ndio wahanga wakuu wa fujo na mizozo duniani

 

Ukiukwaji mwingine mkubwa kabisa unahusu kunyimwa tabaka hilo la watu, haki zake zote na kutofikishiwa misaada ya kibinadamu. Kwa mfano huko Palestina, idadi ya matukio kama hayo ni 3,250 kama yalivyoripotiwa mwaka 2023. Wakati huo huo, matumizi ya nguvu za kijeshi duniani yameongezeka mara tatu na mahitaji ya dharura ya misaada ya kibinadamu yanapuuzwa sana.

Ulimwengu ulikuwa haujawahi kuwa hatari sana kwa watoto kama ilivyotokea mwaka 2023. Shirika hilo lisilo la kiserikali linasema kwamba idadi ya uhalifu uliofanywa wakati wa migogoro ulifikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa mwaka huo.