Waandamanaji Ufaransa wataka kusitishwa tamasha litakalomshirikisha waziri wa Israel
(last modified Fri, 08 Nov 2024 12:16:48 GMT )
Nov 08, 2024 12:16 UTC
  • Waandamanaji Ufaransa wataka kusitishwa tamasha litakalomshirikisha waziri wa Israel

Waungaji mkono Palestina nchini Ufaransa wametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kufuta tamasha lililopangwa kufanyika Novemba 13 mjini Paris, ambapo waziri wa fedha wa utawala haramu wa Israel mwenye misimamo mikali, Bezalel Smotrich, anatazamiwa kuhudhuria.

Waandamanaji walikusanyika kwenye Uwanja wa Trocadero karibu na Mnara wa Eiffel katika mji mkuu, wakitaka serikali ya Ufaransa izuie tamasha lililoandaliwa na Taasisi ya 'Israel Daima'.

Waandamanaji hao waliimba walisikika wakito nara kama vile "Smortrich Hatakikani Paris kwa Tamasha"  na "Mapambano ya Palestina Yadumu".

Walioshiriki katika maandamano hayo walikuwa wamebeba  bendera za Palestina na Lebanon pamoja na mabango yaliyosema "Serikali za Magharibi Zinahusika na Mauaji ya Kimbari huko Gaza" na " Smotrich ni Muuaji."

Wanasiasa wa Ufaransa, mashirika ya kiraia ya Kiyahudi yanayopinga Uzayuni na marabi wanaopinga Uzayuni pia walijiunga na maandamano hayo.

Rabi wa Kiyahudi alishikilia bendera akisema "Marabi wa kweli daima wanapinga Uzayuni na taifa la Israeli."

Mwezi uliopita, Thomas Portes, mbunge kutoka chama cha upinzani cha Ufaransa Haisalmu Amri, aliwasilisha ombi rasmi kwa Idara ya Polisi ya Paris kufuta ushiriki wa Smotrich katika tamasha hilo.

Mnamo Novemba 4, mashirika sita ikiwa ni pamoja na Ligi ya Haki za Kibinadamu ya Ufaransa ilitoa taarifa ya pamoja ikitaka tukio hilo kughairiwa.