Jul 25, 2016 17:06 UTC
  • McKinney: Israel inahusika na mashambulizi ya kigaidi Ulaya

Mbunge wa zamani katika Kongresi ya Marekani amefichua nafasi ya utawala wa kizayuni wa Israel katika mashambulizi ya kigaidi yanayofanyika barani Ulaya.

Cynthia McKinney ameashiria mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika hivi karibuni katika nchi za Ulaya na kusema kuwa, kuwepo kwa mpiga picha wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad,  Richard Gutjahr ambaye pia ni mume wa mwanasiasa na mbunge wa zamani wa Bunge la Israel katika matukio yote mawili ya kigaidi ya Nice huko Ufaransa na Munich nchini Ujerumani ni ishara kwamba, Tel Aviv ina mkono katika mashambulizi hayo.

Cynthia McKinney ameongeza kuwa, haiwezekani kukubali kwamba, mpigapicha huyo aliyapiga picha kwa sadfa tu matukio ya mashambulizi yote mawili ya kigaidi. 

Mkanda wa video uliotegemewa na mbunge wa zamani wa Marekani, Cynthia McKinney kuelekeza kidole cha tuhuma kwa Israel unamuonesha  Richard Gutjahr, mume wa Einat Wilf mwanachama wa zamani wa Bunge la Israel (Knesset) katika mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Nice na Munich.

Watu wasiopungua 84 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi la Nice nchini Ufaransa.

Ijumaa iliyopita pia watu 10 waliuawa mjini Munich baada ya kushambuliwa kwa risasi na wengine 27 wamejeruhiwa.   

Tags