Shambulizi la bomu dhidi ya hospitali Pakistan laua 50
https://parstoday.ir/sw/news/world-i12853-shambulizi_la_bomu_dhidi_ya_hospitali_pakistan_laua_50
Makumi ya watu wameuawa katika mlipuko wa bomu uliolenga hospitali kuu ya mji wa Quetta, kusini magharibi mwa Pakistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 08, 2016 03:38 UTC
  • Shambulizi la bomu dhidi ya hospitali Pakistan laua 50

Makumi ya watu wameuawa katika mlipuko wa bomu uliolenga hospitali kuu ya mji wa Quetta, kusini magharibi mwa Pakistan.

Habari zinasema kuwa, watu 52 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya bomu kuripuka katika chumba cha dharura cha hospitali hiyo ambacho kilikuwa na mawakili. Imearifiwa kuwa mawakili hao walikuwa katika hospitali hiyo kuchukua mwili wa mwenzao aliyeuawa kwa kupigwa risasi masaa machache kabla ya mripuko huo kutokea.

Sarfaraz Bugti, rais wa zamani wa chama cha mawakili wa Balochistan ameuawa mapema leo kwa kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana katika mji wa Quetta.

Maafisa usalama katika eneo la mripuko mjini Quetta, Pakistan

Sarfaraz Bugti, Waziri wa Mambo ya Ndani wa eneo la Balochistan amelaumu utepetevu wa maafisa usalama na vyombo vya kiintelijinsia kwa hujuma hiyo ya bomu hospitalini.

Hadi tunaenda mitamboni, hakuna kundi lolote lililokuwa limekiri kuhusika na shambulizi hilo wala mauaji ya wakili mashuhuri katika eneo hilo Sarfaraz Bugti.

Ramani ya Pakistan na nchi zinazopakana nayo

Mwishoni mwa mwezi Machi mwa huu, watu 52 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotikisa mji wa Lahore, kaskazini mashariki mwa Pakistan.

Polisi ya Pakistan ilisema mlipuko huo ulitokea nje ya Bustani ya Gulshan Iqbal mjini Lahore, katika mkoa wa Punjab, ambao ni moja ya mikoa salama isiyoshuhudia hujuma za kigaidi.