Hollande amtabiria ushindi Hillary Clinton katika uchaguzi wa Rais Marekani
Rais wa Ufaransa anaamini kuwa mwanamke ndiye atakayechaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
Akizungumzia kampeni za uchaguzi zinazoendelea nchini Marekani, Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema kuwa kwa kuzingatia chunguzi mbalimbali za maoni zilizofanyika nchini humo, tunaweza kutabiri kuwa Hillary Clinton ndiye atakayeibuka na ushindi.
Rais wa Ufaransa ameongeza kuwa Ulaya haiwezi kuitegemea Marekani katika kudhamini usalama wa mipaka yake, bila kujali kwamba Hillar Clinton mgombea wa chama cha Democrat amekuwa na misimamo ipi au amefanya nini?
Kuhusu suala la kujiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, Rais wa Ufaransa amesisitiza kuwa harakati huru za raia wa nchi za Ulaya huko Uingereza ambazo ni moja ya misingi ya Umoja wa Ulaya hazipaswi kutumbukia hatarini.Tafiti mbalimbali za maoni zinaonyesha kuwa Hillary Clinton mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani anaungwa mkono na wapiga kura kwa asilimia 44 huku Donald Trump mgombea wa chama cha Republican akiungwa mkono kwa asilimia 37. Uchaguzi wa Rais nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba 8 mwaka huu.