Trump ateua 'Jibwa Kichaa' kuwa Waziri wa Ulinzi Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i20602-trump_ateua_'jibwa_kichaa'_kuwa_waziri_wa_ulinzi_marekani
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua aliyekuwa Kamanda mwandamizi wa jeshi la Marekani Jenerali James Mattis kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 02, 2016 04:34 UTC
  • Trump ateua 'Jibwa Kichaa' kuwa Waziri wa Ulinzi Marekani

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua aliyekuwa Kamanda mwandamizi wa jeshi la Marekani Jenerali James Mattis kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.

Akizungumza hapo jana mjini Cincinnati, Trump alisema tumemteua "Jibwa lenye Kichaa" kuwa Waziri wa Ulinzi lakini habari hizi atazitangaza rasmi Jumatatu ijayo.

Mattis mwenye umri wa miaka 66 na ambaye amekuwa akitangaza wazi wazi kuwa haungi mkono makubaliano ya nyuklia ya Iran, ni maarufu nchini Marekani kwa kuendesha operesheni kadhaa nyeti katika nchi za Iraq na Afghanistan.

James Mattis

Kadhalika afisa huyo wa zamani wa jeshi la Marekani anajulikana kwa jina maarufu la "Jibwa lenye Kichaa" amekuwa akifanya safari za mara kwa mara katika nchi za Kiarabu na utawala haramu wa Israel kwa ajili ya kuendesha njama dhidi ya Iran.

Hayo yamejiri siku chache baada ya Trump kuwateua watu wenye chuki na Waislamu na Uislamu kushika nyadhifa nyeti katika serikali yake.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump

Miongoni mwa maadui hao wa Uislamu ni afisa mstaafu katika Jeshi la Marekani Luteni Jenenrali Michael Flynn aliyeteuliwa na Trump kuhudumu kama mshauri wa usalama wa taifa, licha ya historia yake ya  kutoa matamshi makali dhidi ya Uislamu.

Mwengine ni Seneta Jeff Session ambaye alitangaza kuunga mkono msimamo wa Trump wa kuzuia Waislamu kuingia nchini Marekani. Seneta huyo mwenye chuki za kidini dhidi ya Waislamu na Uislamu ameteuliwa na Trump kuwa mwanasheria mkuu wa Marekani.