Mar 06, 2017 07:44 UTC
  • Radiamali ya Congresi ya Marekani kwa mchezo mpya wa Trump

Wabunge wa chama cha Democrat katika Congresi ya Marekani wamekosoa ombi la rais wa nchi hiyo aliyeitaka Congresi hiyo kuchunguza madai yake kwamba mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na timu yake ya kampeni ya uchaguzi wa rais yalisikilizwa kwa siri.

Rais Donald Trump wa Marekani amedai kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama aliamuru kusikilizwa mazungumzo ya simu ya timu ya kampeni ya uchaguzi ya Trump katika jengo la Trump. Wabunge wa chama cha Democrat wamemtuhumu Trump kuwa ameanzisha njama nyingine zisizo na msingi ili kuzipotosha fikra za waliowengi kuhusu masuala ambayo yamekuwa yakiisumbua serikali yake  katika wiki hizi za mwanzo za utawala wake. Katika upande mwingine wawakilishi wa chama cha Republican pia wamemtaka Rais Trump aziruhusu kamati za kiintelijinsia za bunge la seneti na la wawakilishi kufanya kazi zao kwa uhuru. Wakati huo huo vyama vyote viwili yaani Democrat na Republican vimetamka wazi kuwa madai yaliyotolewa na Rais Trump hayatasalia bila jibu. 

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama aliyetuhumiwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump

Hii ni katika hali ambayo ikulu ya Marekani (White House) hadi sasa haijawasilisha ushahidi wowote wa kuthibitisha madai hayo ya Trump huku maafisa wa serikali iliyotangulia ya Obama wakikadhibisha madai hayo na kuyataja kuwa yasiyo na msingi. 

Tags