Nchi za Kiislamu zataka bidhaa za Israel zisusiwe kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i2692-nchi_za_kiislamu_zataka_bidhaa_za_israel_zisusiwe_kimataifa
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito wa kususiwa bidhaa za zinazozalishwa na utawala haramu wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 08, 2016 22:18 UTC
  • Nchi za Kiislamu zataka bidhaa za Israel zisusiwe kimataifa

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito wa kususiwa bidhaa za zinazozalishwa na utawala haramu wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya nchi za Kiislamu duniani imetoa wito kwa jamii ya kimataifa na nchi wanachama kususia na kupiga marufuku bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Taarifa hiyo imetolewa katika Kikao cha tano cha dharura cha wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichomalizika juzi katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Maudhui kuu ya mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya wawakilishi 500 wa nchi 57 za Kiislamu ilikuwa "Palestina na Quds Tukufu".

Aidha OIC ilitoa wito wa kuwepo himaya kamili ya kisiasa, kidiplomasia na kisheria ili kuhakikisha Wapalestina wanapata haki zao.

Mwezi uliopita mamia ya Wapalestina waliandamana katika Ukingo wa Magharibi wakitaka bidaa za utawala haramu wa Israel zisusiwe.

Ujenzi wa vitongoji vya Wayahudi katika ardhi za Palestina huwa na maana ya kutwaliwa mashamba, nyumba na ardhi za Palestina, kwa msingi huo kila mwaka Wapalestina wengi wamekuwa wakilazimishwa kuhama na kuwa wakimbizi kutokana na siasa hizo za kibaguzi za Israel.

Ni kwa sababu hiyo pia ndiyo maana jumuiya kadhaa za kimataifa zikaanzisha kampenzi iliyopewa jina la 'Susia Israel' ili kulalamikia siasa hizo za kutaka kujitanua za utawala wa kibaguzi wa Israel.