Warusi wengi wana mtazamo chanya kuhusu Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32620-warusi_wengi_wana_mtazamo_chanya_kuhusu_waislamu
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa nchini Russia yameonyesha kuwa raia wengi wa nchi hiyo wana mtazamo chanya kuhusu Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 02, 2017 22:04 UTC
  • Warusi wengi wana mtazamo chanya kuhusu Waislamu

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa nchini Russia yameonyesha kuwa raia wengi wa nchi hiyo wana mtazamo chanya kuhusu Waislamu.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Levada yameonyesha kuwa asilimia 59 ya raia wa Russia wana hisia chanya kuhusiana na Waislamu.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, ni asilimia 13 tu ya Warusi wana mtazamo hasi na mbaya juu ya Waislamu.

Uchunguzi huo wa maoni umefanywa kwa njia ya mahojianio ya moja kwa moja na taasisi hiyo mnamo mwezi wa Juni mwaka huu wa 2017 na matokeo yake yametangazwa mwezi uliomalizika wa Julai.

Waislamu wa Russia wakiwa katika ibada ya Sala

Taasisi ya Levada imelinganisha matokeo ya uchunguzi iliofanya na uchunguzi kama huo uliofanywa mwishoni mwa mwaka 2012 na kubaini kuwa katika kipindi hiki, hisia hasi za raia wa Russia kuhusiana na Waislamu zimepungua kwa asilimia nne.

Uislamu ni dini ya pili yenye wafuasi wengi nchini Russia na watu milioni 20 hadi 23 raia wa nchi hiyo ni Waislamu.

Kiwango hicho ni sawa na asilimia 10 hadi 13 ya idadi ya watu wote wa nchi hiyo.../