Russia yatishia kuishambulia Israel iwapo itavunja makubaliano ya kusitisha vita Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32838-russia_yatishia_kuishambulia_israel_iwapo_itavunja_makubaliano_ya_kusitisha_vita_syria
Naibu kamanda wa vikosi vya jeshi la Russia huko kusini mwa Syria ameutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba, uwapo utakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kusini mwa Syria, Moscow inajua nini inapaswa kufanya.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Aug 07, 2017 22:33 UTC
  • Russia yatishia kuishambulia Israel iwapo itavunja makubaliano ya kusitisha vita Syria

Naibu kamanda wa vikosi vya jeshi la Russia huko kusini mwa Syria ameutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba, uwapo utakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kusini mwa Syria, Moscow inajua nini inapaswa kufanya.

Alexei Cuzin amesema kuwa, Tel Aviv haipasi kuanzisha mashambulizi dhidi ya ardhi ya Syria na inawajibika kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.

Ameongeza kuwa, kuhusu makubaliano hayo, Russia imeipa Israel masharti kwamba iwapo itachukua uamuzi wa kufanya mashambulizi huko kusini mwa Syria, Moscow ambayo ndiyo inayosimamia utekelezaji wa makubaliano hayo itakabiliana na Israel.

Kamanda wa Jeshi la Russia, Syria

Kanali ya Pili ya televisheni ya Israel imeripoti kuwa, Tel Aviv ilikuwa na matarajio kwamba, sambamba na kupelekwa askari wa Russia huko kusini mwa Syria, jeshi la nchi hiyo na wanapambano wa Hizbullah wangeondoka katika maeneo ya mpaka wa utawala huo na Syria lakini matarajio hayo hayakutimia na Wasyria wametangaza waziwazi kuwa wataendelea kuwepo katika eneo hilo la mpakani.